May 15, 2018



Baada ya Yanga kuanza vibaya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo, amesema kuwa ni lazima washinde mechi yao ijayo dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda.

Yanga ilianza hatua hiyo kwa kufungwa mabao 4-0 na USM Alger ya Algeria ambapo keshokutwa Ju­matano itacheza na Rayon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Katika michuano hiyo, Yanga imepangwa Kundi D pamoja na USM Alger ya Algeria, Rayon Sport (Rwanda) na Gor Mahia kutoka Kenya.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Zahera alisema: “Hatukuweza kufanya vizuri kwenye mchezo wa kwanza kutokana na ku­tokuwa na kikosi kamili kwa sababu wengine waligoma, nadhani mnajua, na mmesikia hilo.

“Lakini hivi sasa tunajipanga kwa mchezo ujao kuhakikisha tunash­inda, tangu nimekuja hapa nime­kuwa nikiwafuatilia wapinzani wetu tuliokuwa nao kundi moja, lakini kilichokuwa kinanifanya nisiweze ku­fanikiwa kuwaandaa vizuri wachezaji ni kutokana na wengine kukosekana.

“Hivi sasa wachezaji wangu wapo vizuri na matumaini yangu ni kuona tunafanya vizuri tukianza na mchezo huo dhidi ya Rayon hapa nyumbani.”

4 COMMENTS:

  1. Ijapokuwa walikataa kushirikiana na Mnyama kwa kushangiliana lakini itabidi Simba kuyapuuza hayo na kushangilia watani wetu ambao wanahitaji msaada isipokuwa wanashindwa kuomba msaada huo wasionekane wahitaji

    ReplyDelete
  2. Simba inatupasa kuungana na kuweka ushabiki pembeni na kuwashangilia Yanga

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  3. Hatuhiji kusaidiwa cc wenyewe tunatoxha nyie endeleen tu kuvua nguo huko mitaan mgumba kabemba mimba mate mtaa mxima

    ReplyDelete
  4. Akuanzae mmalize! Walikataa kutushangilia na sisi ni mwendo huo huo tu!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic