May 3, 2018



Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles, amefunguka kiaina kuhusiana na taarifa zilizoenea kuhusiana na kuahirishwa kwa Mkutano Mkuu wa Yanga uliokuwa umepangwa kufanyika Jumamosi ya Mei 5 2018.

Akizungumza kupitia Radio EFM, Mkwasa amesema kuwa subira inahitajika kupata majibu rasmi kuhusiana na mkutano huo kama umeahirishwa au haujaahirishwa.

Mkwasa ameeleza kuwa leo watatoa jibu rasmi juu ya suala hilo ambapo wameitisha kikao na Waandishi wa Habari kitakachofanyika majira ya saa 6 mchana.

Kikao hicho kitaeleza mustakabali mzima juu ya mkutano huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na wapenzi pamoja na mashabiki wa Yanga ambao ulilenga zaidi kubadili mfumo wa uendeshwaji ndani ya klabu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic