May 6, 2018



Na George Mganga

Klabu ya Simba inashuka Dimbani Jumapili ya leo ikiialika Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Ndanda ambayo ipo kwenye hatihati ya kushuka daraja itakuwa inakutana na Simba iliyoukosa ubingwa wa ligi kwa takribani miaka mitano.

Kuelekea mchezo huo, uongozi Simba kupitia kwa Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, umesema kuwa mechi hiyo itakuwa ni ngumu na hawahitaji kuwadharau Ndanda.

Djuma ameeleza kuwa hawapaswi kuwachukulia poa kutokana na mazingira waliyonayo kwenye msimamo wa ligi ukizingatua hivi sasa watakuwa wanapambana kukwepa nafasi ya kuteremka daraja.

Ndanda inaingia kibaruani ikiwa na alama 23 katika nafasi ya 15 ya msimamo wa ligi, wakati Simba wakiwa vinara na alama 62 kileleni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic