May 27, 2018





Wakati mshambuliaji Gareth Bale ndiye aliyepata maksi nyingi zaidi katika mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kipa wa Liverpool, Loris Karius ndiye kapata za chini zaidi.

Bale amepata maksi 8/10 licha ya kwamba aliingia katika mechi hiyo kuchukua nafasi ya Isco, akafanikiwa kufunga mabao mawili na Madrid kushinda kwa mabao 3-1.

Kipa huyo amepata maksi 3/10 na ndiye amepata maksi za chini zaidi ya wote katika mchezo wa lao.


Karius alianza kufanya makosa wakati akirusha mpira ambao ulitua mguuni mea Karim Benzema na kuandika bao la kwanza.

Akarudia kosa kama hilo kwa kushinda kudaka shut la Bale liliandikisha bao la tatu. Kabla Bale alifunga bao la pili kwa tik tak.

Baada ya mechi hiyo, Karius alizunguka upande wa mashabiki wa Liverpool akiwaomba radhi kwa alichokifanya.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic