Uongozi wa Singida United umemtangaza Tiba John George kuwa mchezaji wake kwa kusaini naye mkataba wa miaka mitatu.
George amejiunga na matajiri hao wa mjini Singida akitokea Ndanda FC kutoka Mtwara iliyojikwamua kuepuka kushuka daraja msimu uliomalizika.
Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, amemtambulisha mchezaji huyo mbele ya Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Hotel ya Naura Springs, jijini Arusha.
George atakuwa sehemu ya kikosi cha Singida katika michuano ya SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza kesho jijini Nairobi, Kenya.
Hivi dirisha la usajili limefunguliwa? Maana naona timu za Simba, Azam FC, Singida United, Yanga wanatangaza kusajili. Na wachezaji hao hawana mikataba au wananunua mikataba ya wachezaji?
ReplyDeleteProtas-Iringa