May 25, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umezidi kupiga danadana kuhusiana na kuongeza wachezaji watatu watakaokipa nguvu kikosi chao kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kupitia Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa, amesema kuwa bado hawajafikia maamuzi ya kuweka wazi wachezaji ambao wamepanga kuwaongeza kikosini na muda utakapofika watawataja rasmi.

Kwa mujibu wa radio One kupitia Spoti Leo, Mkwasa ameeleza kuwa kwa sasa wanamalizia mechi za ligi ikiwamo ya leo dhidi ya Ruvu Shooting na itakayofuata watacheza na Azam FC.

"Bado hatujatoa taarifa rasmi kuhusiana na wachezaji hao, wakati mwafaka ukifika tutafanya hivyo, nawomba muendelee kusubiri" alieleza Mkwasa.

3 COMMENTS:

  1. Wanini wachezaji wakukodi ambapo Yanga imesheheni mastaa pamoja na Hajibu. Kumbuka kuwa kanzu ya kuazima haisitiri matako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kazu ya kuazima haisitiri matako hahahahahhahahaha

      Delete
  2. Hizo ndizo porojo za Mkwasa,majukwaani anasema mengine ili kuwashusha pressure mashabiki lakini uwanjani unakwenda kukutana kikosi kile kile cha dhihaka.Mfumo huu ataenda nao hivyohivyo hadi Siku inawadia.,atapanga kikosi cha kucheza na keko rangers.Anatudhihaki huy

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic