May 25, 2018


Uongozi wa klabu ya Toto Africans umetangaza kuitisha kikao maalum kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi Jumapili ya wiki hii mkoani Mwanza.

Klabu hiyo iliyoshuka daraja, imepanga kufanya kikao hicho maalum kitakachopanga mikakati ya Uchaguzi Mkuu ambao utafanyika hivi karibuni.

Kupitia Mwenyekiti wa klabu hiyo, Godwin Michael, amesema kuwa tayari maandalizi ya kikao kuelekea Jumapili yanaenda vizuri .

Uongozi umeeleza unaingia kufanya uchaguzi mkuu kupata watu ambao wataisaidia klabu hiyo kuweza kurejea Ligi Kuu Bara baada ya kushuka mpaka ligi daraja la pili.

Toto ilishuka rasmi daraja kutoka Ligi Kuu Bara mpaka kwanza msimu wa 2015/16 na Mwanza ikawa inawakilishwa na Mbao FC ambayo mpaka sasa ipo kwenye ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic