May 7, 2018



Klabu ya soka ya Yanga imeungana klabu ya soka ya Manchester United na mashabiki wengine wa soka duniani kumuombea apone haraka kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson ambaye amefanyiwa oparesheni ya Ubongo.

Kocha huyo mwenye mafanikio makubwa ndani ya United na ligi kuu ya England, jana alifanyiwa upasuaji wa Ubongo (Brain haemorrhage) na kwa mujibu wa klabu yake hiyo ya zamani upasuaji ulienda salama.

Yanga kupitia ukurasa wao wa Instagram wameandika, ”Tunaungana na wapenda soka duniani kote, kukutakia heri na kukuombea urejee kwenye afya njema”, ambapo ujumbe huo umeambatana na picha ya Fergie.

Kwa upande wao Manchester United wamesema upasuaji umefanyika salama kabisa ila kwasasa bado yupo Hospitali kwa mapumziko zaidi chini ya uangalizi wa jopo la madaktari.

2 COMMENTS:

  1. Nami naungana na wanoko wote kuitakia Yanga kipigo chengine cha 4G. Jamaa hawana aibu hata kidogo, wanadhani wakijitetea eti ni teens, mara ni usaliti, mara hali ya uchumi etc. wataonewa huruma. Tana wana bahati, vile vijeba vingekubali kwenda vingepigwa mileledi - bila shaka ingekuwa 2x4G, yaan two SIM cards za 4G.

    ReplyDelete
  2. jamani toka lini Sir Ferguson anaelewa kiswahili? Yanga acheni aibu hii, ... haisaidii kitu hata mkituma salamu haitaondosha ukweli kuwa mlimiminiwa 4 Goals -Nil. Aibu gani hii jamani. Hebu tuwasuburi Gor! Fikiria Gor walivyo na usongo. Sijui watakimbilia wapi kuficha nyuso zao kwa aibu hawa mayebo, ... hata wanyarwanda watawachuna tu bila huruma.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic