May 7, 2018



Baada ya nyota saba wa Yanga wakiwemo Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa kushindwa kuondoka na timu hiyo kwenda Algeria, straika wa zamani wa Simba na Yanga, Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’, amesema wachezaji hao na wenzao ni wasaliti.


Nyota hao ‘waligoma’ lakini kwa aina yake wakitoa udhuru kila mtu kwa mtindo wake lakini nyuma ya pazia ikielezwa wanagoma wakishinikiza walipwe malimbikizo ya mishahara yao.

Yanga Alhamis ya wiki jana kwenda Algeria kushiriki mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi USM Alger mechi ya Kundi D

Wachezaji ambao hawakuondokaondoka na timu ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshishimbi, Ibrahin Ajibu, Thabani Kamusoko na Beno Kakolanya.

Mogella alisema kuwa wachezaji hao ni wasaliti kwani walipaswa kutanguliza maslahi ya nchi halafu mambo mengine yangefuata baadaye.

“Klabu zinapaswa kuwa makini kutimiza mahitaji ya wachezaji hao kama walikubaliana jambo fulani liwe hivi basi watekeleze na si vinginevyo kama haya yanayotokea kwa Yanga.

“Lakini wachezaji wa Yanga nao ni wasaliti sababu walitakiwa kutanguliza mbele maslahi ya klabu kwanza ukiangalia wachezaji ambao hawajaondoka na timu ni wale ambao ni tegemeo,” alisema Mogella.

Naye straika wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ alisema: “Wachezaji wa sasa wanatakiwa kubadilika sababu wamekuwa wakitanguliza maslahi mbele kuliko kazi kama ilivyokuwa zamani.” alisema.

Hata hivyo Yanga imeshindwa kutamba mbele ya USM Alger kwa kukubali kufungwa jumla ya mabao 4-0, mchezo ukipigwa dimba la Julai 5 1962 Jumapili ya jana.

Chanzo: Championi

3 COMMENTS:

  1. Wewe Mogela na Mohammed Hussein ....... mmesahau ya kwenu mlichokifanya wakati wenu, Kama ni kweli hawajalipwa mishahara yao miezi na miezi... usaliti wao nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yamga wapigaji wengi, kupigwa 4G na waarabu tulitegemea mapema, kwani timu iende na viongizi kumi na moja kundi kubwa lote hilo la nini, Salum Mkermi ana msaada gani Yanga kama siyo kupiga hela za wachezaji wanaovuja jasho? Mkutan mkuu uitishwe haraka kuindoa virus kama Mkeremi, Deusdedit, Nsajigwa na eachezaji karibu wote wa kigeni, ishu ya Ngoma naamini kuna watu wanapiga pesa kupitia mchezaji huyo siyo bure haiwezekani mchzaji hana msaada wa timu ila analipwa mshahara mkubwa kwa nini alisajiliwa wkt inajulikana mkorofi

      Delete
    2. Ngoma alisajiliwa ili kuikomoa Simba wasimsajili....ndio bahati nasibu yenyewe yaani pata potea.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic