June 23, 2018


Mshambuliaji aliyekuwa anaichezea Difaa El Jadida ya Morocco, Hamid Ahadad amejiunga na Zamalek SC inayoshiriki Ligi Kuu Misri.

Ahadad ameondoka Jadida ambayo anaichezea Mtanzania, Saimon Msuva aliyojiunga nayo akitokea katika klabu ya Yanga.

Kuondoka kwa Ahadad kunaweza kukampa nafasi kubwa Msuva ya kuzidi kuonesha makali yake ndani ya ligi ya Morocco ambapo hivi sasa wachezaji wapo mapumziko.

Mchezaji huyo amefikia makubaliano na mabosi wa Zamalek kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu utakaomalizika mwaka 2021.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic