June 23, 2018


Real Madrid wana hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Lyon Nabil Fekir, huku Liverpool ikiwa katika hatari ya kumkosa mchezajihuyo mwenye umri wa miaka 24 mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa. (RT France - Mirror)

Arsenal imefanya mazungumzo na mchezaji wa Sevilla na timu ya taifa ya Argentina Ever Banega, kuhusu uhamisho kuelekea Emirates. (Star)

Manchester City na Paris St-Germain wana hamu ya kumsajili mchezaji wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 29 kiungo cha ulinzi - Jerome Boateng. (Sport Bild - Manchester Evening News)

Chelsea wanaelekea kupunguza malipo kwa kumfuta meneja Antonio Conte kwa kutuhumu kwamba hakushughulikia vizur kuuzwa kwa Diego Costa. (Express)

Manchester City wanaelekea kukaribia ufanisi wa usajili wake wa kwanza wa msimu wa joto baada ya mzungumzo mazuri kuhusu mchezaji wa kiungo cha kati wa Napoli Jorginho, 26. (Manchester Evening News)

Manchester City inajitayarisha kuidhinisha mazungumzo kuhusu kandarasi mpya ya mchezaji wa kiungo cha kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, ambaye pia amehusishwana uhamisho kwenda Barcelona. (Sun)

Meneja wa Rangers Steven Gerrard ana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria anayeichezea Roma Umar Sadiq, mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports)

Tottenham wamehusishwa na uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa wa timu ya Nice Alassane Plea, mwenye umri wa miaka 25, huku meneja wa Spurs Mauricio Pochettino akionekana kumpa ushindani Harry Kane. (Foot Mercato - Sun)

Borussia Monchengladbach wameanzisha mazungumzo ya kumsajili Plea, anayeandamwa pia na Tottenham. (Nice-Matin - Talksport)


Liverpool wamedokezewa kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Stoke City na Switzerland Xherdan Shaqiri. (Express)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic