BEKI SIMBA AIPA MTIHANI MGUMU TIMU YAKE
Imeripotiwa kuwa aada ya kushindwa kung'ara katika ligi ndani ya msimu uliomalizika, beki wa Simba, Ally Shomari, amesema atapambana kuonesha utofauti kwenye KAGAME.
Shomari ambaye alisajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar FC kuelekea msimu wa 2017/18, ameeleza kuwa anajipanga vilivyo kujituma katika mashindano hayo ili kumshawishi kocha wake ampe nafasi zaidi.
Ikumbukwe Shomari hakucheza mechi za takribani msimu mzima uliomalizika na nafasi yake ikitumikiwa vilivyo na Shomari Kapombe ambaye alikuja na kasi kubwa baada ya kupona majeraha yake.
Ujio wa mashindano ya KAGAME yanayoanza kutimua vumbi wiki ijayo yataipa mtihani Simba kupitia kocha Masoud Djuma, kuweza kutathimini kiwango chake kama kitaleta ushawishi wa kumpanga kwenye kikosi cha kwanza.
Tayari wachezaji wa Simba wameanza mazoezi jana baada ya kumaliza mapumziko yao kwenye Uwanja wa White Sand uliopo maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.







0 COMMENTS:
Post a Comment