June 23, 2018


Imeripotiwa kuwa Mhubiri mmoja nchini Argentina amewahimiza waumini wa kanisa lake kumlipa takriban $2,000 to atume kikosi cha "mashujaa wa maombi" kuwasaidia Super Eagles kupata ushindi Kombe la Dunia.

Nigeria walichapwa 2-0 na Croatia mechi yao ya kwanza Kombe la Dunia Urusi na katika mchezo wa jana dhidi ya Iceland wakafanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kwa mujibu wa BBC, Nabii wa kujitawaza Tommy Yisa Aika alisema mapema wiki hii kwamba Super eagles walishindwa mechi hiyo ya Croatia kwa sababu walikuwa wanaadhibiwa na Mungu kwa kumteua kocha mzungu, Gernot Rohr.

Shirika la habari la AFP linasema mhubiri huyo sasa anasema Nigeria wanaweza kujikomboa na kuwa taifa la kwanza la Afrika kushinda Kombe la Dunia iwapo mashabiki wa soka watampatia naira 750,000 ($2,092, euro 1,797).

"Ninachohitaji ni malipo kidogo tu, naira 750,000 ndipo nipate vifaa vya maombi vya kuwapa mashujaa wangu wa maombi kama kichochezo," alisema kwenye mahojiano ya runinga, kwa mujibu wa gazeti la Daily Post lililonukuliwa na AFP.

Aika amesema waumini wake maalum wako tayari kuanza kazi, ili "kile kilichoharibiwa kirekebishwe na Super Eagles wapate neema ya Mungu katika michuano hiyo."

Kufuatia ushindi dhidi ya Iceland jana, Nigeria watakutana na Argentina kwenye mechi yao ya mwisho ya Kundi D.

1 COMMENTS:

  1. Wachungaji na Manabii na Maaskofu hizo ndizo zao. AIBU watu wa Mungu kutanguliza fedha kujifanya mpo karibu na Mungu wa watu wote.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic