June 24, 2018


Na George Mganga

Mabao matatu aliyofunga Mshambuliaji wa timu ya taifa ya England, Harry Kane dhidi ya Panama leo yanamfanya mchezaji huyo kufikisha idadi ya mabao matano.

Kane amefanikiwa kufikisha idadi hiyo ya mabao ikimfanya awe mchezaji pekee anayeongoza kwa ufungaji katika michuano ya kombe la dunia inayoendelea hivi sasa huko Urusi.

Mbali na kufikisha idadi hiyo ya mabao, Kane amekuwa mchezaji wa pili kufunga mabao matatu ndani ya mechi moja sawa na Ronaldo aliyefunga idadi hiyo dhidi ya Spain.

Rekodi hiyo ya kipekee kwa Kane inamfanya awe juu katika michuano hii kwa sasa kutokana na kumzidi bao moja Ronaldo aliye na mabao manne.

Mchezaji Romelu Lukaku kutoka Ubelgiji naye amefunga idadi ya mabao sawa na Ronaldo ambaye ana manne.

3 COMMENTS:

  1. Kuna kufunga na kufunga magori katika mechi bora,Kane anamzidi Ronaldo lakini Ukweli ni kuwa Ronaldo amefunga magoli katika mechi bora,kuilinganisha Panama na Hispania ni matumizi mabaya ya fikra.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upo sawa kweli wewe? wangefungwa na panama ungesemaje?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic