Na George Mganga
Mchezaji aliyekuwa akiichezea Gor Mahia FC ya Kenya, Meddie Kagere, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba.
Kagere aliwasili jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo na mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 na kufanikiwa kufikia makubaliano.
Mchezaji huyo aliyeng'ara katika mashindano ya SportPesa Super Cup huku akiwafunga Simba moja ya bao kati ya mawili katika mchezo wa fainali, amemalizana na uongozi wa klabu hiyo mpya akiwa chini ya wakala wake, Patrick Gakumba.
Kagere ameungana na beki kutoka Ivory Coast, Pascal Wawa ambaye naye imeelezwa tayari ameshamalizana na Simba japo bado haijawekwa wazi kama ameshasaini mkataba.
Ujio wa Kagere unaweka wasiwasi nafasi ya Laudit Mavugo kutoka Burundi ambaye hapewi nafasi kubwa ya kuendelea kusalia katika kikosi cha Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Mavugo kila la heri,karibu sana KAGERE,this is SIIIMMBBAAAAAAAAAAA.
ReplyDeleteNaamini Simba wapo makini kweli usajili wa Kagere... Wasije wakalizwa baadaye!!
ReplyDeleteSimba mambo ni 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
ReplyDeleteUsajili wetu Simba mwaka huu utadhani ni uvuvi wa kokoro....
ReplyDeleteHapo mmelamba dume, ila muwe makini kwani mkataba wake na Gor Mahia unaisha mwisho wa July
ReplyDeleteNimesoma mtandao wa Gor Mahia mashabiki wamemtishia kagere kuwa mpira wake utakufa kwa kuwa akuondoka kwa amani na utaratibu mzuri, sasa hivi wanalalamika na kulaumiana ni vurugu tupu kenya wanamshambulia Mo Dewji eti anapesa za mashetani (juju money) wanasema kagere atakuwa kama Dan Nserukuma
ReplyDeleteSiku zote mfa maji haachi kutapatapa,muacheni kagere akajaribu bahati yake Simba,haina sababu yakujenga migogoro baina yake na uongozi,wala msimchukie mo dewj kisa kagere ameliamsha.
ReplyDeleteSimba inahitaji wachezaji wa kuwasajili so wamajaribio
ReplyDeleteChonde chonde Kagere yasimkute ya Dan!! Wanasimba tumuombee abaki na kiwango chake!!!
ReplyDelete