BREAKING: AGGREY MORRIS AONGEZA MKATABA MWINGINE NA AZAM FC
Beki wa klabu ya Azam FC, Aggrey Moris, ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Mchezaji huyo na Azam wamefikia makubaliano ili kuendelea kuimarisha safu yake ya ulinzi zikiwa siku chache zimesalia kuelekea michuano ya KAGAME.
Morris amefunga pingu za maisha na Azam mpaka mwaka 2020 ambapo mkataba wake utakuwa umemalizika.
Beki huyo ameongeza mkataba mwingine na Azam ikiwa ni siku chache matajiri hao watoke kumalizana na beki wa kulia aliyekuwa anaichezea Vipers FC ya Uganda, Nicholas Wadada.
0 COMMENTS:
Post a Comment