June 6, 2018


Mshambuliaji Adam Salamba, ametua mjini Nakuru tayari kuongeza nguvu katika kikosi cha Simba ambacho kimevuka hadi nusu fainali ya michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup.

Simba inatarajia kuchuka dimbani kesho kuivaa Kakamega Homeboyz katika mechi ya nusu fainali ya michuano hiyo katika uwanja wa Afrah, kesho.

Salamba amejiunga na Simba akitokea Lipuli FC na ametua usiku huu na kuungana na wenzake kambini.

Mshambuliaji huyo alibaki nchini Tanzania kutokana na kuwa na matatizo kadhaa ya kifamilia, lakini leo amejiunga na kikosi hicho.

Simba itashuka dimbani saa 7 mchana kuivaa Homeboyz na mechi ya pili ni hiyo ya wawakilishi wengine wa Tanzania, Singida United.







2 COMMENTS:

  1. Ametua Kenya usiku huu na kesho saa saba mchana acheze vizuri? Kila la Kheri.

    ReplyDelete
  2. Ni mchezaji mpya hajaweza kucheza na wenzake itakuwaje kwa kocha?

    Protas Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic