June 6, 2018





Madaktari wa Simba wanaendelea kufanya juhudi kuhakikiha kipa wao, Aishi Manula anacheza mechi ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup.

Simba inatarajia kuchuka dimbani kesho kuivaa Kakamega Homeboyz katika mechi ya nusu fainali ya michuano hiyo katika uwanja wa Afrah, kesho.

Manula ni majeruhi aliumia katika mechi iliyopita dhidi ya Kariobang Sharks baada ya kugongana na beki wake, Paul Bukaba.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema madaktari wamekuwa wakiendelea kufanya juhudi kuhakikisha anakuwa vizuri.

“Wanaendelea kupambana, tuna imani watafanikiwa,” alisema.

Pamoja na Manula, Simba iliambatana na kipa wa akiba kutoka timu ya vijana.


2 COMMENTS:

  1. Mungu abariki Manula apate nafuu awe golini.

    ReplyDelete
  2. Mungu uwe pamoja na Manula ili awe fiti

    Protas Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic