Beki Pascal Wawa katika picha kulia ameonekana akiwa mazoezini leo na wekundu wa Msimbazi katika Uwanja wa Bocco Veterani jijini Dar es Salaam.
Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema tayari wameshamalizana na mchezaji huyo aliyewaji kuicheza Azam FC.
Wawa ameonekana kujifua leo na kikosi cha Simba katika ratiba ya mazoezi ya asubuhi kuelekea michuano ya KAGAME inayotaraji kuanza Juni 29 2018.
Katika mazoezi hayo yaliyofanyika chini ya Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, Wawa ameonekana kuonesha uzoefu na utulivu na kwenda sambamba na kile kocha wake alikuwa akimuelekeza.
Kikosi hicho kwa sasa kitakuwa kinafanya mazoezi mara moja kwa siku baada ya ile ratiba ya kujifua mara mbili kumalizika wiki iliyopita.
Kikosi hicho kwa sasa kitakuwa kinafanya mazoezi mara moja kwa siku baada ya ile ratiba ya kujifua mara mbili kumalizika wiki iliyopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment