TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU: HAZARD VS MADRID, POGBA VS MOURINHO
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 27, alitaka kuuziwa Real Madrid kabla ya fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kuchezwa mwezi Mei.
Baba yake ambaye pia ni mwakilishi wa mchezaji huyo Thierry Hazard anadaiwa kuwasiliana na Real Madrid kabla ya fainali hiyo mjini Kiev, Madrid akisema mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Hazard na Chelsea yamekwama hasa ikizingatiwa hawachezi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao (Marca)
West Ham wako tayari kumpa kiungo wa kati wa England Jack Wilshere mkataba wa mwaka mmoja pekee kwa sababu wana wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kukaa bila majeraha. Wilshere mkataba wake katika klabu ya Arsenal unamalizika majira haya ya joto. (Sun)
Meneja mpya wa klabu ya Everton Marco Silva huenda akaamua kuwauza wachezaji nyota wa klabu hiyo ya Everton - wakiwemo kiungo wa Ufaransa Morgan Schneiderlin, 28, winga wa Congo Yannick Bolasie, 29, beki wa Wales Ashley Williams, 33, na mshambuliaji wa zamani wa England Wayne Rooney, 32. (Star)
Winga wa Newcastle na Scotland Matt Ritchie, 28, yuko tayari kurejea Bournemouth,huku mshambuliaji wa Norway Josh King, 26, naye akitarajiwa kwenda Newcastle. (Sun)
Uhamisho uliopendekezwa wa Riyad Mahrez kutoka Leicester kwenda Manchester City unachelewa kwa sababu kiungo wa kati huyo wa Algeria mwenye miaka 27 anataka alipwe kitita kikubwa cha pesa na Leicester ndipo akubali kuondoka. (Sun)
Mchezaji wa Ubeligji Marouane Fellaini, 30, amefichua kwamba utata kuhusu mkataba wake utatatuliwa hivi karibuni. Kiungo huyo wa kati wa Manchester United atakuwa bila mkataba hivi karibuni lakini amepokea ofa kutoka kwa klabu kadha. (Independent)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 25, amekiri kwamba alikuwa na "matatizo madogo" na meneja wa Manchester United Jose Mourinho msimu uliomalizika hivi majuzi. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita, 23, anatarajiwa kurithi jezi nambari nane iliyokuwa ya Steven Gerrard katika klabu ya Liverpool.(Liverpool Echo)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment