KAGAME YAZIDI KUFANYIWA MABADILIKO, TIMU NYINGINE KUTOKA SUDAN YAONGEZWA
Imeelezwa kuwa klabu aliyojiunga nayo Mtanzania, Thomas Ulimwengu, Al Hilal ya Suda imeongezwa katika mashindano ya Kombe la KAGAME kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Yanga.
Al Hilal wamechukua nafasi hiyo baada ya Yanga kujiondoa kwenye mashindano hayo kwa sababu za kuwapumzisha wachezaji wao kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Wakati Al Hilal wakichukua nafasi ya Yanga, KCCA ya Uganda nao walijiondoa ambapo Vipers SC wamechaguliwa kwa ajili ya kujaza nafasi yao.
Kutokana na mabadiliko hayo, kundi C ambalo ilikuwepo Yanga linakuwa na timu za Simba SC (Tanzania), Dakadaha (Somalia), Al Hilal (Sudan) na St. George (Ethiopia).
Kundi A mabalo KCCA kutoka Uganda ilikuwepo, sasa litakuwa na timu za Vipers SC (Uganda), Azam FC (Tanzania), JKU (Zanzibar) na Kator FC kutoka (Sudan Kusini).
Ehh kumbe na KCCA nao wamewakimbia AZAM
ReplyDeleteMashindano hayana mvuto tena, just wastage of time and energy,bora ndondo cup. Hakuna timu toka rwanda, Burundi na Kenya?
ReplyDelete