Mashabiki wa Simba wametua mjini Nakuru tayari kuisaidia kuishangilia timu hiyo kwa ajili ya michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup.
Simba inatarajia kuchuka dimbani kesho kuivaa Kakamega Homeboyz katika mechi ya nusu fainali ya michuano hiyo katika uwanja wa Afrah, kesho.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema mashabiki hao watakuwa tayari kwa ajili ya kuongeza nguvu.
“Tutaingia fofauti kabisa, haitakuwa Simba ile na tuliona namna tulivyocheza,” alisema.
“Tumejipanga kuingia tofauti na baada ya hapo kuhakikisha tunakwenda fainali na kuchukua ubingwa.
“Mashabiki wataongeza nguvu na baada ya hapo wataisaidia Singida United ambayo itakuwa inaivaa Gor Mahia katika mechi ya jioni,”
Simba itashuka dimbani saa 7 mchana kuivaa Homeboyz na mechi ya pili ni hiyo ya wawakilishi wengine wa Tanzania, Singida United.
Safi sana
ReplyDeleteMungu yupo pamoja na nanyi Wekundu. Ikiwa wao waliobakishwa kuzomea na kuzomea yso ichukulieni chachu ta kunyanyua morali.
ReplyDelete