June 16, 2018


Wakati Ufaransa ikifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Australia mchana huu, Kylian Mbappe amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo kucheza mchezo wa Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa.

Mbappe amecheza mechi ya kwanza akiwa na umri wa miaka 19 na miezi sita na kutengeneza rekodi ya kipekee kwake kwenye michuano hiyo.

Kinda huyo anayeichezea klabu ya PSG ya Ufaransa ameshiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo mikubwa tangu kuanza kuazishwa kwake.

Mbali na Mbappe, Ufaransa nayo imekuwa timu ya kwanza kushinda mechi zake mbili mfululizo za ufunguzi wa michuano hiyo.

Mwaka 2014 iliibuka na ushindi dhidi ya Honduras nchini Brazil na mwaka huu dhidi ya Australia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic