June 17, 2018


Mchezaji ambaye anamudu vilivyo kucheza nafasi ya beki ya kati, Andrew Vincent, yuko mbioni kutua katika kikosi cha Zamalek kinachoshiriki Ligi Kuu ya Misri.

Dante ambaye msimu uliopita alicheza pacha na Kelvin Yondani kwenye kikosi cha Yanga amemaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo mara baada ya ligi ya msimu uliopita kumalizika.

Beki huyo mwenye rasta alijiunga na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro na mafanikio aliyopata akiwa Jangwani ni kutwaa kombe moja la Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17.

Dante amesema kuwa mpaka sasa ana asilimia 80 za kutua katika ardhi ya Misri na kujiunga na Zamalek iliyomaliza ligi kuu ya nchini humo nafasi ya nne, kufuatia mazungumzo mazuri yanayoendelea baina yao.

 “Yanga waliniita hivi karibuni na kuniomba tufanye mazungumzo lakini niliwaambia mambo ya kifedha yakiwa tayari tutakaa kwani pamoja na kumaliza mkataba mimi bado natambulika ni mchezaji wa Yanga. Hata kama nitakamilisha dili langu la kwenda nje bado wao ndiyo wanatakiwa kunithibitisha.

“Nashukuru Mungu mazungumzo yangu na Waarabu yana matumaini kwa zaidi ya asilimia 80, hivyo kama mambo yataendelea hivi ninaimani nitakuwa na nafasi nzuri sana ya kwenda kuangalia changamoto mpya nje ya Tanzania japo Yanga wakiwahi nitaangalia mahitaji yao kwangu kwani wao ndiyo walezi kwa sasa,” alisema

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic