NTOTA LIVERPOOL AWASILI TURIN KUMALIZANA NA JUVENTUS
Kiungo wa klabu ya Liverpool, Emre Can, amewasili jijini Turin, Italia kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya tayari kuungana na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini humo, Juventus.
Mjerumani huyo alijiunga Liverpool Julai 2014 akitokea Bayern Leverkusen inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani
Mapema Juni 8 2018 mabosi wa Liverpool walitangaza kuwa baada ya mkataba wa mchezaji huyo kumalizika msimu huu wa majira ya joto atakuwa huru kusajiliwa na klabu nyingine itakayomuhitaji.
Kiungo huyo ameichezea Liverpool jumla ya michezo 167 huku wa mwisho ukiwa dhidi ya Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo walipoteza kwa mabao 3-1.
Can anatarajiwa kusaini mkataba na Juventus ambayo iliondolewa pia na Real Madrid katika hatua ya nusu fainali ya UEFA katika dakika za mwisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment