SIMBA YAAMBULIA USHINDI WA TATU UHAI CUP DODOMA
Na George Mganga
Kikosi cha timu ya vijana cha Simba kimefanikiwa kuwa mshindi namba 3 wa michuano ya Uhai CUP ilivyokuwa ikifanyika Uwanja wa Chuo kikuu jijini Dodoma baada ya ushindi wa mabao 4-3 kwa njia ya matuta dhidi ya Azam FC.
Ushindi huo umepatika mara baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuamuriwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Simba wakifanikiwa kupata 4 huku Azam wakipata 3.
Bao la Simba ndani ya dakika 90 lilifungwa na Yahya Mbegu katika dakika ya 7 ya mchezo na la kusawazisha kwa Azam likiwekwa kimiani na Paul Peter kwenye dakika ya 33.
Baada ya dakika 90 kumalizika na upigaji wa penati kuanza, Simba walifanikiwa kupata 4 huku Azam wakipata 3.
Unapotuambia mshindi wa tatu kawa nani tuambie mshindi wa hicho kikombe ni nani aisee sio unapendelea klabu yako ya Simba buana.
ReplyDelete