June 17, 2018


Na George Mganga

Aliyekuwa mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Eliuta Mpepo, amejiunga rasmi na klabu ya Singida United kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Singida waliomaliza Ligi Kuu Bara wakiwa tano bora wamemtambulisha rasmi mchezaji huyo kupitia kwa Mkurugenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga.

Mpepo amewasili Singida akiwa anamudu vyema kucheza nafasi takribani zote za nafasi ya ushambuliaji na akitarajiwa kukipa nguvu kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu.

Mpepo ameungana na wachezaji wapya waliosajiliwa na Singida wakiwemo Habibu Kyombo aliyetokea Mbao FC, Tiber John George kutoka Ndanda na wengineo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic