June 20, 2018





Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul anayewaniwa kwa udi na uvumba na timu ya Azam FC, ameshindwa kujiunga na timu hiyo hadi pale atakaporejea kocha mpya wa timu hiyo raia wa Uholanzi Hans van Der Plujim  arejee kutoka kwake Ghana ambapo ameenda kwa ajili ya mapumziko ya muda mfupi.

Tangu Juma Abdul amalize mkataba wake wa kuitumikia Yanga mwishoni mwa msimu uliyopita, fununu kubwa zilikuwa ni juu ya usajili wake mpya katika klabu ya Azam FC ambao walidaiwa kumuhitaji kwa udi na uvumba.

Abdul amesema, usajili wake na Azam umekwama kutokana na kutoafikiana baadhi ya makubaliano yake na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo, jambo ambalo kwa sasa linamfanya amsubirie kocha mpya wa timu hiyo Hans Plujim ambaye alihitaji huduma yake arudi.

“Ni kweli Azam walinihitaji kupitia kwa kocha wao mpya Hans Plujim lakini kwa sasa sijamalizana nao kwani kuna baadhi ya mambo ambayo hatujaelewana jambo ambalo limetufanya tumsubirie yeye hadi atakaporudi ili tuje kuona kama tutaelewana ili nijiunge nao rasmi.

“Ujuwe mimi sijahitaji kwenda Azam isipokuwa kocha Hans, yeye ndiye alinihitaji nikatoe huduma huko na tukakubaliana namna atakavyoniwezesha ili nijiunge Azam, lakini nimekutana na baadhi ya viongozi wao naona kama kuna mambo tumeshindwa kuelewana hivyo nitajiunga nao mara baada ya kocha kurejea na kunihakikishia makubaliano yetu ya awali yanafikiwa,” alisema Abdul.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic