June 26, 2018



Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo kwa kushirikiana na SportPesa imetangaza washindi wa kwanza wa promosheni ya mwezi mmoja ya Amsha Amsha na Airtel Money na ushinde ambayo ilizinduliwa Juni 14, mwaka huu.


Zawadi kutoka SportPesa ni pamoja na jezi za Simba na Yanga, simu za smartphone, tiketi za bure za Ligi Kuu Bara msimu ujao, TV na ving’amuzi kutoka StarTimes.



Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza washindi hao, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmando alisema kuwa droo ya kupata washindi hao imesimamiwa na kuchezesha kwa wazi na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ambayo ndiyo wenye jukumu la kusimamia Michezo yote ya bahati nasibu hapa nchini.
"Kama mlivyoona hapa kwa siku ya leo, droo yetu imechezesha kwa uwazi na hii inamaanisha kila mteja anayo fursa ya kuwa mshindi ," alisema Mmbando.

Washindi hao wametangazwa na zawadi zao pia kutangazwa hivyo kuwafanya wengine ambao hawakuwa wamecheza kuanza kuona kwamba kweli zawadi zimeanza kutolewa.

SportPesa ndio kampuni ya kubeti inayoongoza kwa sasa katika masuala ya michezo ya ubashiri nchini hasa kwa upande wa michezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic