June 26, 2018


Wakati mkongwe Aggrey Morris akisaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Azam FC, kiungo wake Salum Abubakar 'Sure Boy' naye ameongeza miaka miwili.

Sure Boy amefikia makubaliano hayo ya kuongeza mkataba wa miaka miwili ili kuendelea kutoa huduma yake ndani ya matajiri hao wa jiji la Dar es Salaam.

Azam wamedhamiria kuboresha mikataba ya wachezaji wao ili kujiweka fiti kuelekea mashindano ya KAGAME kuanzia Juni 29 2018 pamoja na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kwa kuongeza mkataba huo, sasa Sure Boy ataendelea kusalia Azam mpaka mwaka 2020.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic