June 26, 2018


Na George Mganga

Wakala wa mchezaji wa Gor Mahia FC, Patrick Gakumba, amefunguka na kusema mazungumzo baina yake na mabosi wa Simba kuhusiana na Meddie Kagere yanaenda vizuri.

Gakumba amewasili jana jijini Dar es Salaam akiwa na Kagere tayari kukamilisha mazungumzo na mabosi wa Simba kwa ajili ya kumsajili straika huyo ambaye ni gumzo nchini Kenya.

Akizungumza na Radio EFM, Gakumba ameelea kuwa mazungumzo yake na Simba yanaenda vizuri na akisema ni kweli Simba wana nia naye huku akiomba subira iwepo mambo yatakuwa wazi hapo baadaye.

Gakumba amesema kila kitu kinaenda sawia na uwezekano mkubwa wa Simba na na mchezaji kumalizana upo kutokana na nia yao ya dhati ya kumuhitaji mchezaji huyo.

Mchezaji huyo ambaye yupo kwenye mazungumzo na Simba atakuwa amezima rasmi ndoto za Yanga ambao awali walikuwa wakihusishwa kufanya naye mazungumzo ya kutaka kumsajili.

4 COMMENTS:

  1. Jamaa anajifanya shabiki kavalia njano kifuani kumbe anampeka Kagere rangi nyekundu na nyeupe. Pesa ndiyo kila kitu.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic