Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) imeshindwa kuwahukumu wachezaji wa timu ya taifa ya Uswisi, Granit Xhana na Xherdan Shaqir kutokana na aina yao ya ushangiliaji.
Hapo awali iliripotiwa kuwa Xhaka na Shaqiri wamefungiwa kucheza mechi mbili za michuano ya Kombe la Dunia kutokana na aina ya ushangiliaji wao waliouonesha kwa ishara ya kukunja mikono "Eagle Style' dhidi ya Serbia.
Ushangiliaji huo uliweza kuzua mjadala FIFA ukielezwa kuhusishwa na masuala ya kisiasa ambayo yamekuwa yakipigwa vita katika mchezo wa soka na baadaye kutoka ripoti zilizoeleza kuwa FIFA imewafungia wachezaji hao.
Lakini kamati hiyo baada ya kukaa chini na kujadiliana kuhusiana na hukumu yao imebainika hawana makosa yoyote na sasa wapo huru kuendelea na ratiba ya michuano hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment