June 27, 2018


Tarehe kama ya leo miaka kadhaa iliyopita alizaliwa Mlinda Mlango wa mabingwa wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara, mabingwa mara 27, klabu ya Yanga, Beno Kakolanya.

Wakati akisherehekea kuongeza mwaka mwingine leo, Kalonya amemtaja kipa wa kimataifa anayemshabikia na kuukubali uwezo wake ambaye vilevile anashiriki katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Kakolanya amemtaja kipa wa timu ya taifa ya Ujeruman, Manuel Neuer kuwa ndiyo kipa wake bora akihusudu ubora wake ndani ya Uwanja pale anapozipigania timu zake.

Neuer ambaye ambaye anaichezea pia klabu ya Bayern Munich inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani, anamshawishi Kakolanya kujituma zaidi kwenye Uwanja kutokana na umahiri wake akiwa Uwanjani.

Kakolanya hajapata nafasi ya kukichezea kikosi cha Yanga kwa takribani msimu mzima kutokana na majeraha aliyoyapata mwanzoni mwa msimu wa 2017/18 na kuepelekea nafasi yake kuchukulia na Mcameroon, Youthe Rostand.

Saleh Jembe Blog inamtakia kila la kheri Kakolanya katika maisha yake ya soka, na ikimuomba azidi kujituma zaidi ili kutimiza ndoto za maisha yake.

CHANZO: RADIO ONE






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic