YANGA BADO INAUMIZA KICHWA KUWABAKIZA WACHEZAJI HAWA WALIOMALIZA MIKATABA
Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuingia kambini kesho Juni 26, inaelezwa kuwa uongozi wa klabu hiyo unaumiza kichwa kuhusiana na kuwabakiza wachezaji wake waliomaliza mikataba.
Yanga ambayo imekuwa ikipitia kipindi kigumu hivi sasa kutokana na kuyumba kiuchumi, haijaweka wazi mpaka sasa kuhusiana na wachezaji wake ambao mikataba yao imeshamalizika.
Hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Mpito, Abassi Tarimba, alisema kuwa klabu imeshaanza usajili wa kimyakimya huku ikifanya mazungumzo na wachezaji ambao inawahitaji kuweza kuendelea nao.
Wakati Yanga wakifanya mazungumzo na wachezaji, taarifa zilizoripotiwa hivi karibuni zinaeleza kuwa mchezaji wake, Mzambia Obrey Chirwa, ameondoka klabuni hapo na kutimkia Ismailia ya Misri na ikielezwa kuwa tayari ameshamalizana kwa kujiunga nayo.
Baadhi ya wachezaji ambao wameshamaliza mikataba Yanga ni Kelvin Yondani, Juma Abdul, Hassan Kessy, Vincent Andrew, Said Makapu, Emmanuel Martin, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Geofrey Mwashiuya na Ben Kakolanya.
Kiosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini kesho kuanza maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya, mchezo ambao utafanyika tarehe 18 Julai huko Nairobi.
Hapo ndio opo dalili njema?
ReplyDelete