June 25, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linaanza rasmi kutoa mafunzo ya mfumo mpya wa usajili leo unaojulikana kwa jina la TFF FIFA CONNECT.

Mafunzo ya mfumo huu yanaanza kwa ngazi kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kupitia semina ambazo zitawakilishwa na viongozi wa timu husika zinapaswa kupewa elimu hiyo kiundani.

Kwa mujibu wa Ofisa wa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, alisema mfumo huo wa usajili ni wa kitofauti tofauti na ule wa zamani ambao ulizoeleka na wengi.

Semina ya mafunzo hayo inafanyika katika makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo mitaa ya Karume, Ilala, Dar es Salaam.

Baada ya semina kwa ngazi ya klabu za Ligi Kuu Bara, kesho itaendelea tena kwa ngazi ya Ligi Daraja la Kwanza na kuhitimishwa keshokutwa Jumatano kwa Ligi Daraja la Pili.


1 COMMENTS:

  1. Simba na Yanga fanyeni juu chini mtume wawakilishi muache visingizio

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic