June 16, 2018


Imeelezwa kuwa mlinda mlango wa Singida United, Peter  Manyika, hana furaha ndani ya klabu hiyo kutokana na kutotimiziwa stahiki zake kwenye vipengele cya mkataba wake.

Taarifa zinaeleza kuwa wakati Manyika akiingia mkataba na Singida United kuna baadhi ya vipengelea vilijazwa ambavyo mpaka sasa havijatimizwa juu yake.

Imeelezwa kuwa kwa mujibu wa wakala wake, ambaye ni baba yake mzazi, Manyika Peter, amesema kuwa mwanae aliingia makubaliano kadhaa katika vipengele vya mkataba aliosaini na klabu hiyo lakini vimevunjwa.

Kutokana na hali hiyo, inaelezwa Manyika hana furaha ndani ya Singida na anaweza akavunja mkataba wake kisha kutimkia mahala pengine.

Kumekuwa na tetesi kuwa timu yake ya zamani, Simba tayari imeshaanza mazungumzo ya kuweza kumrejesha kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu uliomalizika wa 2017/18.

Aidha Azam FC nao wamehusishwa kusaka saini ya kipa huyo ambaye aliiwezesha Singida United kuwa mshindi wa tatu kwenye michuano ya SportPesa Super Cup iliyofanyika nchini Kenya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic