July 6, 2018


Kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, uongozi wa Lipuli umefanikiwa kumnasa aliyewahi kuwa beki wa Lipuli FC, William Lucian maarufu kama Gallas akitokea Ndanda Fc ya Mtwara.

Gallas ameungana na Matola huko Iringa baada ya kufikia mwafaka wa mazungumzo kwa kusaini kandarasi ya mwaka mmoja.



Lipuli imeendelea kuonesha dhamira kuwa ina nia ya kupigania kikombe cha Ligi msimu kutokana na kuzidi kukiboresha kikosi chake kabla ya ligi kuanza mwezi Agosti 2018.

Gallas atakuwa anaungana pia na mshambuliaji aliyewahi kuichezea Yanga, Paul Nonga ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic