July 6, 2018


Na George Mganga

Wakati kikosi cha Yanga kikiwa kambini hivi sasa kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC utakaopigwa Julai 18 2018 jiji Nairobi Kenya, Kocha Dylan Kerr amesema machache kuelekea mechi hiyo.

Kerr ambaye aliwahi kuinoa Simba miaka kadhaa iliyopita akisaidia na Suleiman Matola, ameeleza kuwa watajipanga vilivyo kuelekea mechi hiyo kutokana na Yanga kuwa na njaa ya kupata alama tatu.

Kerr amesema anajua Yanga tangu waangukie kwenye michuano ya Shirikisho hajawapata ushindi wowote zaidi ya kufungwa na MC Alger ya Algeria pia kwenda sare dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, atahakikisha wanapigania kushinda.

Kocha huyo ameweka bayana kuwa katika mashindano ya KAGAME waliyonayo hivi sasa ni sehemu mojawapo ya maandalizi kukiweka kikosi chao sawa kabla hawajarejea nchini kwao Kenya kwa ajili ya kujifua zaidi.

Kutokana na Yanga kuwa na kiu ya ushindi, Kerr amewaheshimu kwa kueleza mechi hiyo haitakuwa rahisi kwasababu kila timu itahitaji kupata matokeo katika mechi hiyo ili kuweza kusonga mbele katika hatua inayofuata.

"Mechi haitakuwa rahisi kwasababu Yanga hawajapata ushindi wowote mpaka sasa, tutajipanga kuhakikisha tunaweza kushinda ili kusonga mbele, kwa sasa tupo kwenye mashindano ya KAGAME, ni moja ya sehemu ya maandalizi yetu" alisema Kerr.

Ukiachana na Yanga, Gor Mahia Fc nayo haijapata matokeo ya alama tatu zaidi ya sare mbili dhidi ya MC Alger na Rayon Sports ya Rwanda.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic