July 6, 2018Mjumbe aliyekuwa ameteuliwa na uongozi wa Yanga ili kuisaidia kupitia mkutano mkuu uliofanyika hivi hivi karibuni, Abdallah Bin Klebu, amejiondoa kwenye nafasi hiyo.

Klebu amefikia maamuzi ya kujiondoa kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kiafya hivyo kushindwa kumpa nguvu ya kuitendea haki nafasi hiyo.

Mbali na tatizo la kiafya, Klebu amesema pia majukumu ya kikazi yanambana hivyo hataweza kushughulika kama Mjumbe kwenye kamati hiyo maaluma ambayo ilikuwa inampa majukumu ya kuwa chanzo cha kuisaidia Yanga katika wakati huu mgumu inaopitia.

Taarifa zinasema kwa mujibu wa barua aliyoiandika na kuituma kwenye makao makuu ya Yanga Juni 26 2018, imeeleza kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na sababu tajwa hapo juu.

Kleb alichaguliwa kuwa sehemu ya Wajumbe watakaokuwa wanaisaidia Yanga wakati wa mpito ambao sasa kama klabu inapitia kipindi kigumu ikiwa imeyumba kiuchumi, ameamua kujiweka pembeni.

3 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV