June 19, 2019


Imeripotiwa kuwa klabu ya Simba imegoma kutoka kiasi cha fedha ambacho Nkana Red Devils wanakitaka ili kumuachia mchezaji wao Walter Bwalya.

Taarifa za ndani zinasema Nkana wanahitaji kiasi cha shilingi milioni 800 za kitanzania jambo ambalo limekuwa ni gumu kuzitoa.

Uongozi wa juu wa Simba kupitia kwa Ofisa Mtendaji wake, Crescentius Magori, umesema kwa fedha hiyo hawataweza kumsajili Bwalya na badala yake watamsaka mchezaji mwingine.

Imeelezwa kuwa Magori amefunguka kwa kusema Nkana wanadai fedha kubwa tofauti na uwezo wa mchezaji mwenyewe ulivyo kitu ambacho kinaleta ugumu kumnunua.

Tetesi za Bwalya kutua Simbazimeanza muda mrefu lakini mpaka sasa pande zote mbili hazijaelewana juu ya usajili wake.

16 COMMENTS:

  1. Welldone simba,mil 800 sio ya kiwango cha bwalya.mpo makini.

    ReplyDelete
  2. mpeni hati mnyaturu atoe hela ya uxajili

    ReplyDelete
  3. SOKONI HANA THAMANI HIYO WELL DONE VIONGOZI SIMBA HUO UTAKUWA NI UFUJAJI WA PESA

    ReplyDelete
  4. mwacheni akae kwanza maana ni msimu mmoja tu hata yeye anatamani kuhama mtamchukua kama kagere, ngoja amalizie mkataba kwan bado mwaka mmoja tu

    ReplyDelete
  5. Simba kwa ushauri wa bure kabisa wasije wakafanya makosa ya kukosa kumsajili Chirwa wa Azam. Nnaimani atakuja kuwa msaada mkubwa kimataifa hata lighi ya ndani yaani ni dodo iliyolala mchangani inasubiri muokotaji.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chirwa hana kiwango hicho na hana hadhi ya kuchezea Simba

      Delete
  6. Duh hiyo pesa ukiwa serious unapata wachezaji watatu wa maana toka Brazil

    ReplyDelete
  7. Tulisikia mtashindana na timu kubwa kwenye usajili hivi ndo kushindana na al ahaly

    ReplyDelete
  8. Tulisikia mtashindana na timu kubwa kwenye usajili hivi ndo kushindana na al ahaly

    ReplyDelete
  9. Tulisikia mtashindana na timu kubwa kwenye usajili hivi ndo kushindana na al ahaly

    ReplyDelete
  10. Mshambuliaji wa maana wa kuichezea simba ni Kodjo Laba, ikiwa kuna uwezekano wa kumpata na sio bwalya, hana msaada tunaoutaka

    ReplyDelete
  11. ha ha ha, mikia bwana Hamna jipya bwalya kawashinda tatizo pesa!!!!

    ReplyDelete
  12. Hela zenu za madafu mtampata wapi bwalya, poleni sana mikia sc

    ReplyDelete
  13. Hela zenu za madafu hamuwezi kumpata bwalya poleni sanaaaaa

    ReplyDelete
  14. Hela Hamna nyie ya kumpa bwalya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic