July 6, 2018


Wakati lawama zikishuka juu yake kutokana na kutoonesha kiwango kizuri msimu uliopita, imeelezwa kuwa kipa wa Yanga, Mcameroon Youthe Rostand ameuomba uongozi wake umpe chake aweze kuondoka.

Taarifa zilizo chini ya kapeti zinaeleza Rostand amekuwa hana furaha ndani ya Yanga kufuatia uwepo wa tetesi nyingi ambazo amekuwa akizipata kuwa anaweza akaondoshwa na kipa mwingine kusakwa ili achukue nafasi yake.

Kufuatia hatua hiyo, taarifa zinaeleza Rostand amewaomba mabosi wake wampe fedha za kuvunja mkataba ili awe huru na akasake mahala pengine pa kuchezea.

Rostand alisajiliwa kutoka African Lyon ambayo tayari imeshashuka daraja na kuanza vizuri akiwa na mabingwa hao wa kihistoria kwenye Ligi Kuu Bara wakiutwaa ubingwa mara 27, imekuwa ikielezwa anaweza akaachwa.

Taarifa kutoka ndani Yanga zinaeleza kuna uwezekano mkubwa timu ukaleta kipa mwingine kutoka Congo, mpango ambao unaelezwa kufanywa na Kocha wake, Mkongomani, Mwinyi Zahera.

2 COMMENTS:

  1. kwanini huyu bundi anawatesa hv yanga

    ReplyDelete
  2. TAARIFA AMEKUPA AKILIMALI? ENDELEA KUUNGAUNGA TAARIFA TU BRO, MMEDHIBITIWA TRIP HII

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV