July 19, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba umemtangaza rasmi kocha wao mpya, Mbelgiji Patrick Aussems, tayari kuanza kazi ya kuiandaa timu kuelekea mashindano ya Ligi Kuu Bara.

Simba wameingia makubaliano ya mkataba wa mwaka mmoja na Aussems akiwa anachukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre ambaye alimaliza muda wake.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mabosi wa Simba kugoma kumuongezea mkataba Lechantre ambaye alipewa timu kwa muda wa miezi sita pekee na baada ya kumalizika wakaacha naye.

Aussems amesaini mkataba huo mbele ya Makamu Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah maarufu kama Try Again, sambamba na Kaimu Makamu wa Urais, Idd Kajuna pamoja na Waandishi wa Habari.

Kocha huyo amewahi kuzinoa timu kadhaa za Afrika ikiwemo AC Leopards ya Congo, KSA Cameroon ya Cameroon, ES Troyes AC ya Ufaransa na zingine zilizopo  je ya Afrika.

Simba wamefikia hatua ya kumpa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuridhishwa na CV zake hivyo kuona anastahili kukinoa kikosi hicho ambacho kimeshiriki michuano ya SportPesa Super CUP na KAGAME bila ya Kocha Mkuu.

Wakati Aussems akimwaga wino, kikosi cha Simba kinatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi unaotaraji kuanza Agosti 22.

8 COMMENTS:

  1. Hawa simba wanafanya mambo yao kwa uoga mno!hivi kweli kocha mwenye CV nzuri kama hiyo n wa kumpa mwaka (msimu)mmoja?au kwa vile wamezoea timua timua ya makocha

    ReplyDelete
  2. PICHA LA KUTISHA

    ReplyDelete
  3. We Yohana issue za SSC hazikuhusu tuachie wenye timu.pambaneni na halli zenu huko jangwani

    ReplyDelete
  4. Simba hii inajitofautisha na klabu nyingine katika ukanda huu wa mashariki na kati ya Afrika, mambo yanafanyika kwa weledi mkubwa, timu ina malengo na inatafuta njia la kufikia malengo hayo, na ndio maana wanaliimarisha benchi la ufundi, wachezaji wenye uwezo mkubwa wanasajiliwa, wanabadili muundo wa uendeshaji....halafu wanapeleka timu kwenye mashindano sio kubahatisha, na kutegemea miujiza ya Mungu, na visingizio ooh mara refa, ooh hoteli, ooh mara figisu figisu. Huu ni mfano wa kuigwa. Na pia wanawapasha wapenzi kila hatua, kwa uwazi

    ReplyDelete
  5. Kumpa kocha mwaka mmoja si waliongea kwanza? Sasa wewe ulitaka wampe mkataba mrefu wakati wenyewe wamekubaliana? Nafikiri wana malengo makubwa zaidi.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  6. Watanzania tuna matatizo hiyo sio siri na tatizo letu kubwa kama tutalitafutia muarubaini basi tutatoka kama kumeza mate,tatizo lenyewe ni kwamba hatupo waaminifu na serious katika utumishi. Sasa kitu kinacho nipa hamasa kubwa kwa Timu ya Simba hivi sasa basi hakuna kama Simba kuwa chini ya usimamizi wa Mohamed Mo. Na hamasa zangu na matarajio ya kuamini yakuwa SIMBA chini ya usimamizi wa Mo itatisua hazipo yakwamba labda Mo ana uwezo wa pesa peke yaje hapana bali kubwa zaidi ni uwezo wa Mo kiakili na nizamu katika masuala ya management. Kama viongozi waliokuwepo sasa pale Simba wapo kweli kawa ajili ya kuiletea simba maendeleo ya kweli basi ni kumpa Mo ushirikiano mubashara na hayo yakifanyika basi SIMBA na wanasimba si walaumu hata kidogo wakikaa tayri mkao wa kula. .Mungu ndie mpangaji lakini tunatarajia makubwa kutoka kwa Simba na kwa uwezo wa Mungu yatakuwa, Amen.

    ReplyDelete
  7. Huyo Kocha hawamuanini, hiyo cv ni ndogo sana ndio maana wanampa as a trial, 1 yr contract ili iwe rahisi kuvunja mkataba kama ni mbovu, that is a great thinking

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic