July 27, 2018


Na George Mganga

Aliyekuwa Meneja wa timu ya Yanga, Hafidhi Saleh, amebadilishiwa wadhifa wake na sasa atakuwa Coordinator huku nafasi yake ikichukuliwa na aliyekuwa Nahodha, Nadir Haroub ''Cannavaro''.

Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni mwezi mmoja pekee umesalia kuelekea pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu Bara kufunguliwa mnamo Agosti 22 2018.

Cannavaro amechukua nafasi ya Saleh kutokana na kujitoa kwake ndani ya klabu hiyo ambayo ameichezea kwa muda mrefu na akipata mafanikio makubwa.

Kutokana na kukabidhiwa majukumu hayo, Cannavaro sasa anakuwa ametundika rasmi daruga la kucheza kambumbu na badala yake atakuwa anahusika na kukiongoza kikosi cha Yanga kutokana na majukumu aliyokabidhiwa.

Yanga itashuka dimbani Jumapili ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza dhidi ya Gor Mahia FC katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

3 COMMENTS:

  1. KLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI INAWEZEKANA MTANDAO HUU UMESUKWA KWA MUDA MREFU...UNAMUHUSISHA KOCHA MWINYI ZAHERA, HIVI HUYU KOCHA ATAWEZAJE KUKATAA BEKI AMBAYE ANAKUJA KUZIBA MAPENGO YA NAMBA 2 NA TANO? UNAACHA WACHEZAJI, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA...BEKI NAMBA 2 NA 5, WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10, 11, KIUNGO NAMBA 6....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA..

    ReplyDelete
  2. Kaka mkubwa hongera kwa kupata cheo cha umeneja, ila utembee nakauli ya magu usifanye sherehe anapo kuteuwa,kwamaana umekuja na bundi kwenye mfuko wakijani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic