ZAHERA SASA MAMBO SAFI, APATA VIBALI VYA KAZI YANGA
Na George Mganga
Mabosi wa klabu ya Yanga wamethibitisha rasmi kuwa Kocha wake, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amepata vibali vya kufanya kazi nchini.
Tangu Zahera awasili Dar es Salaam amekuwa akijumuika na kikosi cha Yanga katika mazoezi pekee na kushindwa kuwa sehemu ya benchi la ufundi kutokana na vibali vya kazi kukosekana.
Mambo sasa yamenoga Yanga ambapo juhudi za viongozi wa klabu hiyo walizidi kupigania vibali hivyo na hatimaye vimefanikiwa kupatikana ambapo wameeleza keshokutwa Jumapili Zahera atakuwepo kwenye benchi la ufundi dhidi ya Gor Mahia.
Mkongo huyo atakuwa anakaa kwenye benchi hilo kwa mara ya kwanza tangu achukua mikoba ya aliyekuwa Kocha Mkuu Yanga, Mzambia, George Lwandamina ambaye alitimka kimyakimya kurejea kwao baada ya mambo kutoenda sawia baina yake na mabosi wake.
Zahera sasa ataiongoza Yanga katika mchezo huo wa mkondo wa pili dhidi ya Gor Mahia akiwa sambamba na Noel Mwandila ambaye ni Kocha Msaidizi.
KLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI INAWEZEKANA MTANDAO HUU UMESUKWA KWA MUDA MREFU...UNAMUHUSISHA KOCHA MWINYI ZAHERA, HIVI HUYU KOCHA ATAWEZAJE KUKATAA BEKI AMBAYE ANAKUJA KUZIBA MAPENGO YA NAMBA 2 NA TANO? UNAACHA WACHEZAJI, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA...BEKI NAMBA 2 NA 5, WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10, 11, KIUNGO NAMBA 6....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA..
ReplyDelete