July 1, 2018


Liverpool imeanza tena mazungumzo na Lyon kwa ajili ya kiungo mshambuliaji Nabil Fekir, 24. (Sunday Mirror)

Lakini Manchester United pia inamuhitaji mchezaji huyo. (La Progres - via Sunday Express)

Chelsea inatarajia kumtangaza meneja wa zamani wa Napoli Maurizio Sarri kuwa meneja wao mpya juma lijalo. (Talksport)

Tottenham wanampango wa kumnyakua kiungo mshamuliaji wa River Plate na timu ya taifa ya Colombia, Juan Quintero, 25. (La Nueva - via 90min)

Leicester City wamemteua Jacques Bonnevay kuwa meneja msaidizi wakati Michael Appleton akiondoka. (Leicester Mercury)

Mlinda mlango Thibaut Courtois yuko tayari kuondoka Chelsea ikiwa mbelgiji huyo atatimiza ndoto zake kuelekea Real Madrid. (Sunday Mirror)

The Blues wanasuka mipango ya kumnyakua mlina mlango wa Roma Alisson, 25 kwa kitita cha pauni milioni 65 wakiwa na mashaka ya kumpoteza Courtois. (Mail on Sunday)

Mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech, 36, amesema Napoli imeonyesha kumuhitaji lakini yeye ana mpango wa kubaki Emirates. (Calcio Mercato)


Arsenal wanajiandaa kukamilisha mazungumzo kuhusu kumsajili kiungo mshambuliaji wa Uruguay Lucas Torreira, 22 kutoka Sampdoria juma lijalo. (Mail on Sunday)

Liverpool hawana mpango na kiungo mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio, 22, pia mchezaji mwenzake Lucas Vazquez.(Marca)

Juventus sasa inaongoza katika kuwania sahihi ya Sergej Milinkovic-Savic, 23 kutoka Lazio. (Tuttosport - via Star on Sunday)

Manchester United huenda ikamchukua beki wa AC Milan, Leonardo Bonucci, 31 kutokana na timu hiyo kufungiwa kushiriki mashindano ya ulaya. (Gazzetta dello Sport - via Sun on Sunday)


Meneja wa Ajax Erik ten Hag amethibtisha kuwa kiungo mshambuliaji Hakim Ziyech atajiunga na klabu nyingine.Roma imekuwa ikimfukuzia mchezaji huyo mwenye miaka 25, sambamba na Liverpool na Everton. (Goal)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic