July 9, 2018



Aliyekuwa kocha wa klabu ya Barcelona ya Hispania, Luis Enrique, ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Hispania baada ya nchi hiyo kung’olewa katika Kombe la Dunia wakati wa kutafuta 16 bora katika michuano inayoendelea nchini Russia.

Kwa mujibu wa mkataba, Enrique ataishika nafasi hiyo kwa miaka miwili. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48, anachukua nafasi ya Hierro aliyepewa jukumu hilo saa 48 kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia Hispania ilipocheza na Ureno.

Kocha wa awali, Julen Lopetegui,  alifukuzwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia baada ya kukubali kuwa kocha wa klabu ya Real Madrid, na kumwacha aliyekuwa mkurugenzi wa michezo,  Fernando Hierro, kukaimu nafasi hiyo.

Enrique aliondoka Barcelona mwishoni mwa msimu wa 2016/17 baada ya kuitumikia miaka mitatu na baadaye kuzitumikia klabu za Chelsea na Arsena.

1 COMMENTS:

  1. ni lini aliwahi kuzitumika arsenal na chelsea kama mchezaji au kocha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic