July 9, 2018




Mambo yamekamilika na mwezi ujao inatarajiwa kuwa ndoa ya mwanasoka Abdi Banda.

Banda anayekipiga katika klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini anatarajiwa kufunga ndoa na Zawadi Saleh Kiba.
Zawadi ni dada wa mwanamuziki nyota nchini, Ally Kiba.


Taarifa zinaeleza tayari Banda amekamilisha kila kitu na wamekubaliana kumaliza jambo hilo mwezi ujao.

“Ndoa na sherehe zote ni mwezi ujao, yaani Agosti na wawili hawa wameafikiana na familia zao zimeridhia,” kilieleza chanzo.

“Kwa sasa, maandalizi mengine yanaendelea na sisi tunasubiri ili tushiriki. Banda yuko Afrika Kusini kazini kwake, lakini amekuwa akiendelea na maandalizi.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic