July 30, 2018


Na George Mganga

Kocha wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, jana alishindwa kuwa sehemu ya benchi la ufundi na badala yake aliendelea kukaa jukwaani wakati kikosi chake kikiwa Uwanjani kucheza dhidi ya Gor Mahia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Zahera mpaka sasa hajafanikiwa kupata vibali vya kufanya kazi nchini licha ya uongozi wa Yanga kutangaza kuwa atakuwepo katika mechi hiyo baada ya kuitisha kikao cha mwisho na wanahabari kunako makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam.

Katika hali ya kushangaza Zahera ameendelea kukitazama kikosi chake kikicheza akiwa jukwaani tangu atue nchini kuchukua nafasi ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina.

Haijulikana mpaka sasa kipi kimekwamisha kuchelewa kupatikana kwa kibali cha kocha huyo ambaye mpaka sasa inaelezwa vibali vyake vinafuatiliwa.

Katika mchezo huo wa mkondo wa pili, Yanga ilikubali kupoteza mara ya pili mfululizo kwa kufungwa mabao 3-2 na kuendelea kusalia mkiani mwa kundi D.




1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic