July 30, 2018



Kocha Mkuu wa Lipuli FC ya mkoani Iringa, Selemani Matola ameibuka na kusema kuwa na wakati mgumu kutokana na ratiba ya mechi zake za awali za ligi atakazoanza nazo.

Ligi Kuu Bara inatarajia kuanza kutimua vumbi Agosti 22, kwa timu zote shiriki kushuka dimbani kuanza msimu mpya wa 2018/19, kuwania kombe lililopo mikononi mwa Simba walilolitwaa msimu uliopita.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Matola alisema kuwa, ligi ya safari hii itakuwa ngumu na upinzani wa hali ya juu kutokana na ushindani utakaoku wepo.

“Nina wakati mgumu ninaanza na mechi ngumu ambapo naanza na mechi tatu za ugenini dhidi ya Coastal Union, JKT Ruvu na Simba.

“Baada ya mechi hizo nitakutana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa nyumbani, nimekiandaa kikosi changu kuhakikisha kinafanikiwa kuwa katika kiwango kizuri ili kuleta ushindani,” alisema Matola.

Matola ni kati ya makocha ambao waliofanya vizuri msimu uliopita wa ligi ambapo walimaliza msimu wa ligi katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 38.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic