July 9, 2018


Rais wa Real Madrid Florentino Perez anaripotiwa kuwa tayari amechagua namba ya Eden Hazard ikiwa mchezaji huyo wa Chelsea na Ubegiji atahamia Barnabeu. (Diario Gol via Star)

Nduguye Antonio Conte amedai kuwa meneja huyo mwenye miaka 48 raia wa Italia atabakia Chelsea msimu unaokuja, licha ya kuwepo uvumi kuhusu hatma yake. (Mirror)

Manchester City wameafikia makubaliano ya pauni milioni 60 na Leicester kumsaini Riyad Mahrez huku mchezaji huyo wa umri wa miaka 27 akitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya ndani ya saa 48 zinazokuja. (Mail)


Arsenal wako kwenye mazungumzo na Loriet kuhusu kusainiwa kwa mchezaji huyo wa miaka 19 mfaransa, wa kikosi cha walio chini ya miaka 20 Matteo Guendouzi, (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira 22 ambaye anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya huko Arsenal leo Jumatatu kabla ya kuhama kwake anasema anataka kupata fursa kubwa. (Metro)


Baba yake Mesut Ozil amemtaka kiungo wa kati wa Arsenal kumaliza taaluma yake na Ujerumani baada ya mchezaji huyo wa miaka 29 kulaumiwa kufuatia matokeo mabaya kwenye Kombe la Dunia. (Bild via Talksport)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV